Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu

Zaburi 91

Mwenyezi Mungu mlinzi wetu

Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,

atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.1

Nitasema kumhusu Mwenyezi Mungu, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ninayemtumaini.”

Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,

na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

Atakufunika kwa manyoya yake,

chini ya mabawa yake utapata kimbilio,

uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

Hutaogopa vitisho vya usiku,

wala mshale urukao mchana,

wala maradhi ya kuambukiza

yanayonyemelea gizani,

wala tauni iharibuyo adhuhuri.

Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,

kumi elfu mkono wako wa kuume,

lakini haitakukaribia wewe.

Utatazama tu kwa macho yako

na kuona adhabu ya waovu.

Ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako;

naam, Mwenyezi Mungu ambaye ni kimbilio langu;

basi hakuna madhara yatakayokupata wewe,

hakuna maafa yatalikaribia hema lako.

Kwa kuwa atawaagiza malaika wake kwa ajili yako,

wakulinde katika njia zako zote.

Watakuchukua mikononi mwao,

ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.

Utawakanyaga simba na nyoka wakali,

simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.

Mwenyezi Mungu asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa;

nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu.

Ataniita, nami nitamjibu;

nitakuwa pamoja naye katika taabu,

nitamwokoa na kumheshimu.

Kwa siku nyingi nitamshibisha

na kumwonesha wokovu wangu.”

Source notes (1)
  1. Footnote Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.