Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu

Zaburi 29

Sauti ya Mwenyezi Mungu wakati wa dhoruba

Zaburi ya Daudi.

Mpeni Mwenyezi Mungu, enyi mashujaa,

mpeni Mwenyezi Mungu utukufu na nguvu.

Mpeni Mwenyezi Mungu utukufu unaostahili jina lake;

mwabuduni Mwenyezi Mungu katika uzuri wa utakatifu wake.

Sauti ya Mwenyezi Mungu iko juu ya maji;

Mungu wa utukufu hupiga radi,

Mwenyezi Mungu hupiga radi juu ya maji makuu.

Sauti ya Mwenyezi Mungu ina nguvu;

sauti ya Mwenyezi Mungu ni tukufu.

Sauti ya Mwenyezi Mungu huvunja mierezi;

Mwenyezi Mungu huvunja vipande vipande

mierezi ya Lebanoni.

Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,

Sirioni1 urukaruke kama mwana nyati.

Sauti ya Mwenyezi Mungu hupiga

kwa miali ya radi.

Sauti ya Mwenyezi Mungu hutikisa jangwa;

Mwenyezi Mungu hutikisa Jangwa la Kadeshi.

Sauti ya Mwenyezi Mungu huzalisha ayala,

na huuacha msitu wazi.

Hekaluni mwake wote wasema,

“Utukufu!”

Mwenyezi Mungu huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;

Mwenyezi Mungu ametawazwa kuwa Mfalme milele.

Mwenyezi Mungu huwapa watu wake nguvu;

Mwenyezi Mungu huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.

Source notes (1)
  1. Footnote yaani Mlima Hermoni

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.