Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 98

Mungu Mtawala Wa Dunia

Zaburi.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

kwa maana ametenda mambo ya ajabu;

kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu

umemfanyia wokovu.

Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane

na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.

Ameukumbuka upendo wake

na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;

miisho yote ya dunia imeuona

wokovu wa Mungu wetu.

Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote,

ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;

mwimbieni Bwana kwa kinubi,

kwa kinubi na sauti za kuimba,

kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume:

shangilieni kwa furaha mbele za Bwana, aliye Mfalme.

Bahari na ivume na kila kiliomo ndani yake,

dunia na wote wakaao ndani yake.

Mito na ipige makofi,

milima na iimbe pamoja kwa furaha,

vyote na viimbe mbele za Bwana,

kwa maana yuaja kuhukumu dunia.

Atahukumu dunia kwa haki

na mataifa kwa haki.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.