Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 97

Mungu Mtawala Mkuu

Bwana anatawala, nchi na ifurahi,

visiwa vyote vishangilie.

Mawingu na giza nene vinamzunguka,

haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi.

Moto hutangulia mbele zake

na huteketeza adui zake pande zote.

Umeme wake wa radi humulika dunia,

nchi huona na kutetemeka.

Milima huyeyuka kama nta mbele za Bwana,

mbele za Bwana wa dunia yote.

Mbingu zinatangaza haki yake,

na mataifa yote huona utukufu wake.

Wote waabuduo sanamu waaibishwa,

wale wajisifiao sanamu:

mwabuduni yeye, enyi miungu yote!

Sayuni husikia na kushangilia,

vijiji vya Yuda vinafurahi

kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana.

Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote;

umetukuka sana juu ya miungu yote.

Wale wanaompenda Bwana na wauchukie uovu,

kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake

na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.

Nuru huangaza wenye haki

na furaha kwa watu wanyofu wa moyo.

Furahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki,

lisifuni jina lake takatifu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.