Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 140

Kuomba Ulinzi Wa Mungu

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu;

nilinde na watu wenye jeuri,

ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao,

na kuchochea vita siku zote.

Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka,

sumu ya nyoka iko midomoni mwao.

Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu;

nilinde na watu wenye jeuri

wanaopanga kunikwaza miguu yangu.

Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa,

wametandaza kamba za wavu wao,

wametega mitego kwenye njia yangu.

Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.”

Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.

Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu,

unikingaye kichwa changu siku ya vita:

Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao,

usiache mipango yao ikafanikiwa,

wasije wakajisifu.

Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe

na shida zinazosababishwa na midomo yao.

Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie!

Na watupwe motoni,

katika mashimo ya matope,

wasiinuke tena kamwe.

Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi;

maafa na yawawinde watu wenye jeuri.

Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki,

na kuitegemeza njia ya mhitaji.

Hakika wenye haki watalisifu jina lako,

na waadilifu wataishi mbele zako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.