Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 129

Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.

“Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia,” Israeli na iseme. “Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia, lakini hawajanishinda. Wakulima wamekuwa wakilima mgonngoni kwangu; wametengeneza matuta yao marefu. Yahwe ni mwenye haki; amezikata kamba za waovu.” Wote waaibishwe na kurudishwa nyuma, wale wachukiao Sayuni. Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua, ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda. Wale wapitao karibu wasiseme, “Baraka za Mungu na ziwe juu yako; Tunakubariki katika jina la Yahwe.”

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.