Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 128

Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.

Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake. Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa. Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako. Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa. Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako. Uishi uwaone wana wa wanao. Amani iwe na Israli.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.