Biblia Takatifu
Zaburi 130
Tap a verse to save, highlight, add a note or share it.
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe. Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma. Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa. Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi. Israeli, umtumainie yahwe. Yahwe ni wenye huruma, na yuko tayari kusamehe. Ni yeye ambaye ataikomboa istaeli dhidi ya dhambi zake zote.
Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.