Biblia Takatifu
Zaburi 123
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
Nakuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni. Tazama, kama vile macho ya watumishi watazamapo kwenye mkono wa Bwana wao, na kama macho ya mjakazi yatazamapo mkono wa bibi yake, ndivyo hivyo macho yetu yanamtazama Yahwe mpaka atakapo tuhurumia. Ee Yahwe, utuhurumie, kwa maana tunadhalilishwa sana. Tumeshibishwa mzaha wa wenye kiburi na dharau ya wenye majivuno.
Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.