Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 124

Wimbo wa kwenda kuabudu; wa Daudi.

“Kama Yahwe asingekuwa upande wetu,” Israeli na aseme sasa, “Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu, basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu. Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia. Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha.” Atukuzwe Yahwe, ambaye hajaruhusu tuwe mawindo kwa meno yao. Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka. Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.