Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 122

Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi.

Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.” Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako! Ee Yerusalemu, uliojengwa kama mji uliopangiliwa kwa umakini! Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe. Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. Ombeni kwa ajili ya amani ya Yerusalemu! “Wote wakupendao wawe na amani. Amani iwepo ndani ya kuta zako ili ikutetee, na wawe na amani ndani ya ngome zako.” Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu nitasema, “Amani iwe ndani yenu.” Kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu, nitatafuta mema kwa ajili yako.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.