Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 113

Msifuni Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe; lisifuni jina la Yahwe. Litukuzwe jina la Yahwe, tangu sasa na hata milele. Toka maawio ya jua hata machweo yake, Jina la Yahwe lazima lisifiwe. Yahwe ameinuliwa juu ya mataifa yote, na utukufu wake wafika juu mbinguni. Ni nani aliye kama Yahwe Mungu wetu, aliye na kiti chake juu, atazamaye chini angani na duniani? Humwinua maskini toka mavumbini na kumpandisha muhitaji kutoka jaani, ili amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. Humpa watoto wanamke aliye tasa, humfanya yeye kuwa mama wa watoto mwenye furaha. Msifuni Yahwe!

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.