Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 112

Msifuni Yahwe. Amebarikiwa mtu yule anaye mtii Yahwe, apendezwaye sana na amri zake. Kizazi chake kitakuwa ni chenye nguvu duniani; kizazi cha mcha Mungu kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali; na haki yake itadumu milele. Nuru huangazia gizani kwa ajili ya mtu mcha Mungu; yeye ni wa fadhili, huruma, na haki. Heri atendaye fadhili na kukopesha, afanyaye mambo yake kwa uaminifu. Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele. Haogopi habari mbaya; ni jasiri, akimtumainia Yahwe. Moyo wake ni mtulivu, hana woga, mpaka aonapo ushindi dhidi ya watesi wake. Huwapa masikini kwa ukarimu; haki yake yadumu milele; atainuliwa kwa heshima. Mtu mwovu ataona haya na kukasirika; atasaga meno yake na kuyeyuka; tamaa ya wasio haki itapotea.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.