Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 111

Msifuni Yahwe. Nitamshukuru Yahwe kwa moyo wangu wote katikati ya kusanyiko la wanye haki, na katika mkutano. Kazi za Yahwe ni kuu, zikisubiriwa na wale wazitamanio. Kazi yake ni adhama na utukufu, na haki yake yadumu milele. Hufanya mambo makuu ambayo yatakumbukwa; Yahwe ni mwenye huruma na neema. Huwapa chakula wafuasi wake waaminifu. Siku zote atalikumbuka agano lake. Alionesha uweza wa kazi zake kwa watu wake kwa kuwapa urithi wa mataifa. Kazi za mikono yake ni za kuaminika na haki; maagizo yake yote ni ya kuaminika. Yamethibitika milele, yamefanywa katika uaminifu na vizuri. Aliwapa ushindi watu wake; aliliteuwa agano lake milele; jina lake ni takatifu na lakutisha. Kumcha Yahwe ni mwanzo wa hekima; wale washikao maagizo yake wana uelewa mzuri. Sifa yake yadumu milele.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.