Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 114

Israeli ilipotoka Misri, na nyumba ya Yakobo toka kutoka katika wale watu wa kigeni, Yuda ilifanyika kuwa mahali pake patakatifu, Ufalme wa Israeli. Bahari iliona ikakimbia; Yordani ilirudi nyuma. Milima iliruka kama kondoo waume, vilima viliruka kama wana-kondoo. Ewe Bahari kwa nini ulikimbia? Yordani kwa nini ulirudi nyuma? Milima, kwa nini uliruka kama kondoo waume? Enyi vilima wadogo, kwa nini mliruka kama wana-kondoo? Tetemeka, ee nchi, mbele za Bwana, uweponi mwa Mungu wa Yakobo. Aligeuza mwamba kuwa ziwa la maji, jiwe gumu kuwa chemchem.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.