Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
Zaburi 87
Sifa za Yerusalemu
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.
Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
Mwenyezi Mungu anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.
Mambo matukufu yanasemwa juu yako,
ee mji wa Mungu:
“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu1 na Babeli
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,
nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”
Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,
“Huyu na yule walizaliwa humo,
naye Aliye Juu Sana mwenyewe
atamwimarisha.”
Mwenyezi Mungu ataandika katika orodha ya mataifa:
“Huyu alizaliwa Sayuni.”
Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”
Source notes (1)
- Footnote jina la ushairi la Misri
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.