Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
Zaburi 6
Sala ya kuomba msaada wakati wa taabu
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.
Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako,
wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
Unirehemu Mwenyezi Mungu,
kwa maana nimedhoofika;
Ee Mwenyezi Mungu, uniponye,
kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.
Nafsi yangu ina uchungu mwingi.
Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu, hadi lini?
Geuka, Ee Mwenyezi Mungu, unikomboe,
uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
Hakuna mtu anayekukumbuka
akiwa amekufa.
Ni nani awezaye kukusifu
akiwa Kuzimu1?
Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;
usiku kucha natiririsha
kitanda changu kwa machozi;
nimelowesha kiti changu
kwa machozi yangu.
Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,
yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.
Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,
kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia kulia kwangu.
Mwenyezi Mungu amesikia kilio changu kwa huruma,
Mwenyezi Mungu amekubali sala yangu.
Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
watarudi nyuma na waaibishwe kwa ghafula.
Source notes (1)
- Footnote Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol , yaani Shimo lisilo na mwisho.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.