Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu

Zaburi 113

Kumsifu Mwenyezi Mungu kwa wema wake

Msifuni Mwenyezi Mungu.1

Enyi watumishi wa Mwenyezi Mungu msifuni,

lisifuni jina la Mwenyezi Mungu.

Jina la Mwenyezi Mungu na lisifiwe,

sasa na hata milele.

Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,

jina la Mwenyezi Mungu linapaswa kusifiwa.

Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya mataifa yote,

utukufu wake juu ya mbingu.

Ni nani aliye kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,

Yule aliyeketi kwenye kiti cha enzi huko juu,

ambaye huinama atazame chini

aone mbingu na nchi?

Huwainua maskini kutoka mavumbini,

na kuwanyanyua wahitaji

kutoka lundo la majivu,

huwaketisha pamoja na wakuu,

pamoja na wakuu wa watu wake.

Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,

akiwa mama watoto mwenye furaha.

Msifuni Mwenyezi Mungu.

Source notes (1)
  1. Footnote kwa Kiebrania ni Hallelu Yah ; pia 113:9 .

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.