Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
Zaburi 110
Mwenyezi Mungu na mfalme wake mteule
Zaburi ya Daudi.
Mwenyezi Mungu amwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
Mwenyezi Mungu ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
Askari wako watajitolea kwa hiari
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako1.
Mwenyezi Mungu ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
Bwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
Atakunywa maji katika kijito kando ya njia2;
kwa hiyo atainua kichwa chake juu.
Source notes (2)
- Footnote au vijana wako watakujia kama umande
- Footnote au Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka;
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.