Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu
Malaki 4
Siku ya Mwenyezi Mungu
“Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na watenda maovu watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao. Bali ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini. Kisha ninyi mtawakanyaga waovu, nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
“Kumbukeni Torati ya mtumishi wangu Musa, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote.
“Tazama, nitawapelekea nabii Ilya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Mwenyezi Mungu. Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.