Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu

Ayubu 26

Hotuba ya tisa ya Ayubu

Ayubu anajibu: Utukufu wa Mwenyezi Mungu hauchunguziki

Kisha Ayubu akajibu:

“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!

Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!

Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?

Nayo ni busara gani kubwa uliyoonesha!

Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?

Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?

“Wafu wako katika maumivu makuu,

wale walio chini ya maji,

na wale wanaoishi ndani yake.

Mauti1 iko wazi mbele za Mungu;

Uharibifu2 haukufunikwa.

Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu;

naye huining’iniza dunia mahali pasipo na kitu.

Huyafungia maji kwenye mawingu yake,

hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.

Huufunika uso wa mwezi mpevu,

akitandaza mawingu juu yake.

Amechora mstari wa upeo juu ya maji,

ameweka mpaka wa nuru na giza.

Nguzo za mbingu nazo zatetemeka,

zinatishika anapozikemea.

Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari;

kwa hekima yake alimkata Rahabu3 vipande vipande.

Aliisafisha anga kwa pumzi yake;

kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.

Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake;

tazama jinsi ulivyo mdogo mnong’ono tunaousikia kumhusu!

Ni nani basi awezaye kuelewa

ngurumo za nguvu zake?”

Source notes (3)
  1. Footnote yaani Kuzimu ; Kiebrania ni Sheol
  2. Footnote kwa Kiebrania ni Abadon
  3. Footnote Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani , mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.