Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu

Hosea 3

Upatanisho wa Hosea na mkewe

Mwenyezi Mungu akaniambia, “Nenda, ukaoneshe upendo wako kwa mke wako tena, ingawa amependwa na mwingine naye ni mzinzi. Mpende kama Mwenyezi Mungu apendavyo Waisraeli, ingawa wanageukia miungu mingine na kupenda mikate mitamu ya zabibu kavu iliyowekwa wakfu.”

Basi nilimnunua huyo mwanamke kwa shekeli kumi na tano1 za fedha, pia kwa kiasi kama cha homeri moja na nusu2 ya shayiri. Kisha nilimwambia, “Utaishi nami kwa siku nyingi, hupaswi kuwa kahaba au kuwa na uhusiano wa karibu na mtu yeyote, nami nitaishi na wewe.”

Kwa maana Waisraeli wataishi siku nyingi bila kuwa na mfalme wala mkuu, bila kuwa na dhabihu wala mawe matakatifu, bila kizibau wala miungu ya nyumbani. Baadaye Waisraeli watarudi na kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na Daudi mfalme wao. Watakuja wakitetemeka kwa Mwenyezi Mungu na kwa baraka zake katika siku za mwisho.

Source notes (2)
  1. Footnote Shekeli 15 ni sawa na gramu 170.
  2. Footnote Homeri moja na nusu ni kama lita 330.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu. Copyright © 2018, 2024 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. “Biblica” ni alama ya biashara iliyosajiliwa katika United States Patent and Trademark Office (ofisi ya hataza na alama za biashara Marekani) na shirika la Biblica, Inc. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.