Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 95

Wimbo Wa Kumsifu Mungu

Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha;

tumfanyie kelele za shangwe

Mwamba wa wokovu wetu.

Tuje mbele zake kwa shukrani,

tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu,

mfalme mkuu juu ya miungu yote.

Mkononi mwake mna vilindi vya dunia,

na vilele vya milima ni mali yake.

Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya,

na mikono yake iliumba nchi kavu.

Njooni, tusujudu, tumwabudu,

tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,

kwa maana yeye ndiye Mungu wetu,

na sisi ni watu wa malisho yake,

kondoo chini ya utunzaji wake.

Kama mkiisikia sauti yake leo,

msiifanye mioyo yenu migumu

kama mlivyofanya kule Meriba,1

kama mlivyofanya siku ile

kule Masa2 jangwani,

ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,

ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.

Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,

nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,

nao hawajazijua njia zangu.”

Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,

“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”

Source notes (2)
  1. Footnote Meriba maana yake ni Kugombana.
  2. Footnote Masa maana yake ni Kujaribiwa.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.