Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 87

Sifa Za Yerusalemu

Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.

Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

Bwana anayapenda malango ya Sayuni

kuliko makao yote ya Yakobo.

Mambo matukufu yanasemwa juu yako,

ee mji wa Mungu:

“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu1 na Babeli

miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:

Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,2

nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,

“Huyu na yule walizaliwa humo,

naye Aliye Juu Sana mwenyewe

atamwimarisha.”

Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:

“Huyu alizaliwa Sayuni.”

Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,

“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Source notes (2)
  1. Footnote Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri.
  2. Footnote Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.