Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 39

Maombi Ya Mtu Anayeteseka

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu

na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi;

nitaweka lijamu kinywani mwangu

wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”

Lakini niliponyamaza kimya na kutulia,

hata pasipo kusema lolote jema,

uchungu wangu uliongezeka.

Moyo wangu ulipata moto ndani yangu,

nilipotafakari, moto uliwaka,

ndipo nikasema kwa ulimi wangu:

“Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu

na hesabu ya siku zangu;

nijalie kujua jinsi maisha yangu

yanavyopita upesi.

Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi;

muda wangu wa kuishi ni kama

hauna thamani kwako.

Maisha ya kila mwanadamu

ni kama pumzi.

Hakika kila binadamu ni kama njozi

aendapo huku na huko:

hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili;

anakusanya mali nyingi,

wala hajui ni nani atakayeifaidi.

“Lakini sasa Bwana, nitafute nini?

Tumaini langu ni kwako.

Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote,

usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu.

Nilinyamaza kimya,

sikufumbua kinywa changu,

kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili.

Niondolee mjeledi wako,

nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako.

Unakemea na kuadhibu wanadamu

kwa ajili ya dhambi zao;

unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo:

kila mwanadamu ni kama pumzi tu.

“Ee Bwana, usikie maombi yangu,

usikie kilio changu unisaidie,

usiwe kiziwi kwa kulia kwangu.

Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni,

kama walivyokuwa baba zangu wote,

Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena

kabla sijaondoka na nisiwepo tena.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.