Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 29

Sauti Ya Bwana Wakati Wa Dhoruba

Zaburi ya Daudi.

Mpeni Bwana, enyi mashujaa,

mpeni Bwana utukufu na nguvu.

Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;

mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.

Sauti ya Bwana iko juu ya maji;

Mungu wa utukufu hupiga radi,

Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.

Sauti ya Bwana ina nguvu;

sauti ya Bwana ni tukufu.

Sauti ya Bwana huvunja mierezi;

Bwana huvunja vipande vipande

mierezi ya Lebanoni.

Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,

Sirioni1 urukaruke kama mwana nyati.

Sauti ya Bwana hupiga kwa miali

ya umeme wa radi.

Sauti ya Bwana hutikisa jangwa;

Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.

Sauti ya Bwana huzalisha ayala,

na huuacha msitu wazi.

Hekaluni mwake wote wasema,

“Utukufu!”

Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;

Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.

Bwana huwapa watu wake nguvu;

Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.

Source notes (1)
  1. Footnote Yaani Mlima Hermoni.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.