Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 26

Maombi Ya Mtu Mwema

Zaburi ya Daudi.

Ee Bwana, nithibitishe katika haki,

maana nimeishi maisha yasiyo na lawama;

nimemtumainia Bwana

bila kusitasita.

Ee Bwana, unijaribu, unipime,

uuchunguze moyo wangu

na mawazo yangu;

kwa maana upendo wako

uko mbele yangu daima,

nami natembea siku zote

katika kweli yako.

Siketi pamoja na watu wadanganyifu,

wala siandamani na wanafiki,

ninachukia kusanyiko la watenda mabaya

na ninakataa kuketi pamoja na waovu.

Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia,

naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana,

nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa,

huku nikisimulia matendo yako ya ajabu.

Ee Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi,

mahali ambapo utukufu wako hukaa.

Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi,

wala uhai wangu pamoja na wamwagao damu,

ambao mikononi mwao kuna mipango miovu,

ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa.

Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama;

nikomboe na unihurumie.

Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare;

katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.