Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 138

Maombi Ya Shukrani

Zaburi ya Daudi.

Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote,

mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako.

Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu,

nami nitalisifu jina lako

kwa ajili ya upendo wako

na uaminifu,

kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako

juu ya vitu vyote.

Nilipoita, ulinijibu;

ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.

Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Bwana,

wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako.

Wao na waimbe kuhusu njia za Bwana,

kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.

Ingawa Bwana yuko juu,

humwangalia mnyonge,

bali mwenye kiburi

yeye anamjua kutokea mbali.

Nijapopita katikati ya shida,

wewe unayahifadhi maisha yangu,

unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu,

kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.

Bwana atatimiza kusudi lake kwangu,

Ee Bwana, upendo wako wadumu milele:

usiziache kazi za mikono yako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.