Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 110

Bwana Na Mfalme Wake Mteule

Zaburi ya Daudi.

Bwana amwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

mpaka nitakapowafanya adui zako

kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”

Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;

utatawala katikati ya adui zako.

Askari wako watajitolea kwa hiari

katika siku yako ya vita.

Ukiwa umevikwa fahari takatifu,

kutoka tumbo la mapambazuko

utapokea umande wa ujana wako.1

Bwana ameapa,

naye hatabadilisha mawazo yake:

“Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki.”

Bwana yuko mkono wako wa kuume,

atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.

Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga

na kuwaponda watawala wa dunia nzima.

Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,2

kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

Source notes (2)
  1. Footnote Au: vijana wako watakujia kama umande.
  2. Footnote Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.