Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Nehemia 7

Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”

Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni

(Ezra 2:1-70)

Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:

Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):

Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:

wazao wa Paroshi

2,172

wazao wa Shefatia

372

wazao wa Ara

652

wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu)

2,818

wazao wa Elamu

1,254

wazao wa Zatu

845

wazao wa Zakai

760

wazao wa Binui

648

wazao wa Bebai

628

wazao wa Azgadi

2,322

wazao wa Adonikamu

667

wazao wa Bigwai

2,067

wazao wa Adini

655

wazao wa Ateri (kupitia Hezekia)

98

wazao wa Hashumu

328

wazao wa Besai

324

wazao wa Harifu

112

wazao wa Gibeoni

95

watu wa Bethlehemu na Netofa

188

watu wa Anathothi

128

watu wa Beth-Azmawethi

42

watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi

743

watu wa Rama na Geba

621

watu wa Mikmashi

122

watu wa Betheli na Ai

123

watu wa Nebo

52

wazao wa Elamu

1,254

wazao wa Harimu

320

wazao wa Yeriko

345

wazao wa Lodi, Hadidi na Ono

721

wazao wa Senaa

3,930

Makuhani:

wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua)

973

wazao wa Imeri

1,052

wazao wa Pashuri

1,247

wazao wa Harimu

1,017

Walawi:

wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia)

74

Waimbaji:

wazao wa Asafu

148

Mabawabu wa malango:

wazao wa // Shalumu, Ateri, Talmoni, // Akubu, Hatita na Shobai

138

Watumishi wa Hekalu:1

wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,

wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,

wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,

wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,

wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,

wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,

wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,

wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

wazao wa Nesia na Hatifa.

Wazao wa watumishi wa Solomoni:

wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,

wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.

Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni

392

Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

wazao wa // Delaya, Tobia na Nekoda

642

Na kutoka miongoni mwa makuhani:

wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).

Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. Kwa hiyo, mtawala2 aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.3

Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245. Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245 ngamia 435 na punda 6,720.

Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,0004 za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani. Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu,5 na mane 2,2006 za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.

Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.

Ezra Asoma Sheria

Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,

Source notes (6)
  1. Footnote Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).
  2. Footnote Au Tirshatha : jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70).
  3. Footnote Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
  4. Footnote Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6.
  5. Footnote Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172.
  6. Footnote Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.