Skip to content
BibleKenya

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Yoshua 12

Orodha Ya Wafalme Walioshindwa

Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:

Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.

Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi1 hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi2), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.

Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):

mfalme wa Yeriko

mmoja

mfalme wa Ai (karibu na Betheli)

mmoja

mfalme wa Yerusalemu

mmoja

mfalme wa Hebroni

mmoja

mfalme wa Yarmuthi

mmoja

mfalme wa Lakishi

mmoja

mfalme wa Egloni

mmoja

mfalme wa Gezeri

mmoja

mfalme wa Debiri

mmoja

mfalme wa Gederi

mmoja

mfalme wa Horma

mmoja

mfalme wa Aradi

mmoja

mfalme wa Libna

mmoja

mfalme wa Adulamu

mmoja

mfalme wa Makeda

mmoja

mfalme wa Betheli

mmoja

mfalme wa Tapua

mmoja

mfalme wa Heferi

mmoja

mfalme wa Afeki

mmoja

mfalme wa Lasharoni

mmoja

mfalme wa Madoni

mmoja

mfalme wa Hazori

mmoja

mfalme wa Shimron-Meroni

mmoja

mfalme wa Akishafu

mmoja

mfalme wa Taanaki

mmoja

mfalme wa Megido

mmoja

mfalme wa Kedeshi

mmoja

mfalme wa Yokneamu katika Karmeli

mmoja

mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) 3

mmoja

mfalme wa Goimu katika Gilgali

mmoja

mfalme wa Tirsa

mmoja

wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

Source notes (3)
  1. Footnote Yaani Bahari ya Galilaya.
  2. Footnote Yaani Bahari Mfu.
  3. Footnote Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.