Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
Ezra 2
Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni
(Nehemia 7:4-73)
Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):
Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:
wazao wa Paroshi
2,172
wazao wa Shefatia
372
wazao wa Ara
775
wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu)
2,812
wazao wa Elamu
1,254
wazao wa Zatu
945
wazao wa Zakai
760
wazao wa Bani
642
wazao wa Bebai
623
wazao wa Azgadi
1,222
wazao wa Adonikamu
666
wazao wa Bigwai
2,056
wazao wa Adini
454
wazao wa Ateri (kupitia Hezekia)
98
wazao wa Besai
323
wazao wa Yora
112
wazao wa Hashumu
223
wazao wa Gibari
95
watu wa Bethlehemu
123
watu wa Netofa
56
watu wa Anathothi
128
watu wa Azmawethi
42
wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi
743
wazao wa Rama na Geba
621
watu wa Mikmashi
122
watu wa Betheli na Ai
223
wazao wa Nebo
52
wazao wa Magbishi
156
wazao wa Elamu ile ingine
1,254
wazao wa Harimu
320
wazao wa Lodi, Hadidi na Ono
725
wazao wa Yeriko
345
wazao wa Senaa
3,630
Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua)
973
wazao wa Imeri
1,052
wazao wa Pashuri
1,247
wazao wa Harimu
1,017
Walawi:
wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia)
74
Waimbaji:
wazao wa Asafu
128
Mabawabu wa lango la Hekalu:
wazao wa // Shalumu, Ateri, Talmoni, // Akubu, Hatita na Shobai
139
Watumishi wa Hekalu:1
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
wazao wa Uza, Pasea, Besai,
wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
wazao wa Nesia na Hatifa.
Wazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,
wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
Watumishi wa Hekalu wote na // wazao wa watumishi // wa Solomoni
392
Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
wazao wa // Delaya, Tobia na Nekoda
652
Kutoka miongoni mwa makuhani:
Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.2
Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, ngamia 435 na punda 6,720.
Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,0003 za dhahabu, mane 5,0004 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.
Source notes (4)
- Footnote Yaani Wanethini (pia 2:58, 70 ).
- Footnote Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
- Footnote Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500.
- Footnote Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0. Source: eBible.org. Typeset from the source files; no intended changes to scripture wording. BibleKenya is not endorsed by the rights holder.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.