Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 24

Zaburi ya Daudi.

Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake. Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito. Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake? Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya. Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake. Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia! Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe, mwenye nguvu na uweza; Yahwe, mwenye uweza katika vita. Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia! Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe wa majeshi, yeye ni Mfalme wa utukufu.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.