Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 23

Zaburi ya Daudi.

Yahwe ni mchungaji wangu; sita pungukiwa na kitu. Yeye hunilaza katika majani mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu. Yeye huurejesha uhai wangu; huniongoza katika njia iliyo sahihi kwa ajili ya jina lake. Hata ijapokuwa nikipita katika bonde la uvuli na giza nene, sitaogopa kudhurika kwa kuwa wewe uko pamoja nami; fimbo yako na gongo lako vya nifariji. Wewe waandaa meza mbele yangu katika uwepo wa maadui zangu; umenipaka mafuta kichwa changu na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na uaminifu wa agano vitaniandama siku zote za maisha yangu; nami nitaishi katika nyumba ya Yahwe milele!

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.