Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 82

Zaburi ya Asafu.

Mungu amesimama katika kusanyiko la mbinguni; katikati ya miungu anahukumu. Hata lini mtahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu? Selah Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara. Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu. Hawajui wala hawaelewi; hutembea gizani; misingi yote ya nchi imebomoka. Mimi nilisema, “Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu. Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu.” Uinuke, Ee Mungu, uihukumu nchi, maana unaurithi katika mataifa yote.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.