Biblia Takatifu
Zaburi 70
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; kuleta kumbukumbu.
Uniokoe, Mungu! Yahwe, njoo haraka na unisaidie mimi. Wale wajaribuo kuchukua uhai wangu waaibishwe na kufedheheshwa; warudishwe nyuma na wasiheshimiwe, wale wafurahiao katika maumivu yangu. Warudishwe nyuma kwa sababu ya aibu yao, wale wasemao, “Aha, aha.” Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu asifiwe.” Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.
Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.