Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 67

Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi, wimbo.

Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote. Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani. Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki. Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.