Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 53

Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Mahalath. Maschil ya Daudi.

Mpumbavu husema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wamepotoka na kufanya machukizo; hakuna mmoja atendaye mema. Toka mbinguni Mungu hutazama chini kwa wanadamu kuona kama kuna yeyote mweye akili, amtafutaye yeye. Wote wamekengeuka. Kwa pamoja wamepotoka. Hakuna atendaye mema, hata mmoja. Je, wale wanao fanya uovu hawana uelewa - wale walao watu wangu kana kwamba wanakula mkate na hawamuiti Mungu? Wao walikuwa katika hofu kuu, ingawa hakuna sababu ya kuogopa ilikuwepo hapo; maana Mungu ataitawanya mifupa ya yeyote atakaye kusanyika dhidi yako; watu kama hao wataaibishwa kwa sababu Mungu amewakataa wao. Oh, kwamba wokovu wa Israel ungepatikana Sayuni! Wakati Mungu atakapowaleta watu wake kutoka kifungoni, ndipo Yakobo atashangilia na Israeli itafurahi!

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.