Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Zaburi 13

Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.

Mpaka lini, Yahweh, utaendelea kunisahau? Ni kwa muda gani utauficha uso wako nisiuone? Ni kwa muda gani nitalazimika kuhofu na kuhuzunika moyoni mwangu kila siku? Ni kwa muda gani adui zangu watanishida? Unitazame na unijibu, Yahwe Mungu wangu! Nipe mwanga machoni pangu, vinginevyo nitalala katika mauti. Usimuache adui yangu aseme, “Nimemshinda huyu,” ili kwamba asiweze kusema, “Nimemtawala adui yangu;” la sivyo, maadui zangu watafurahia nitakapo shushwa chini. Lakini nimeamini katika uaminifu wa agano lako; moyo wangu wafurahia katika wokovu wako. Nitamuimbia Yahwe kwa kuwa ameniganga kwa ukarimu kabisa.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.