Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Mithali 9

Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo saba kutoka katika miamba. Ameandaa wanyama wake kwa chakula cha usiku; ameichanganya divai yake; na kuandaa meza yake. Amewatuma watumishi wake kupeleka mialiko na kutoka mahali pa juu sana kwenye mji anaita: “Wale wasiofunzwa waje hapa!” anawaambia wale wasionaufahamu. Njoo, ule chakula, na unywe divai nimeshaichanganya. Acheni njia zenu za kijinga, na mkaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu. Yeyote amrekebishaye mwenye dhihaka hukaribisha matusi na yeyote anayemshutumu mtu mbaya atapata madhara. Usimshutumu mwenye dhihaka, ama atakuchukia; mshutumu mtu mwenye busara, naye atakupenda. Mpe mafundisho mtu mwenye busara, naye atakuwa na busara zaidi; mfundishe mtu mwenye haki, naye ataongeza elimu. Hofu ya Mungu ni chanzo cha hekima na maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu. Maana kwa njia yangu siku zako zitazidishwa na uzima wako utaongezewa miaka. Kama unahekima, unahekima kwako mwenyewe, lakini ukidharau, utaibeba peke yako. Mwanamke mpumbavu anakelele nyingi- hajafunzwa wala haelewi chochote. Anakaa kwenye mlango wa nyumba yake, kwenye kiti cha sehemu ya juu sana ya mji. Anawaita kwa sauti wanaopita karibu, watu wale wanaotembea wima katika njia zao. Wale ambao hamjafunzwa njoni hapa ndani!” anawaambia wale wasio na akili. “ Maji ya kuiba ni matamu na mkate unaoliwa kwa siri unapendeza.” Lakini hajui kwamba wafu wapo pale, wageni wake wapo kwenye vina vya kuzimu.

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.