Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Yeremia 45

Hili ni neno ambalo Yeremia nabii alimwambia Baruku mwana wa Neria. Hii ilitokea wakati alipoandika kwenye kitabu maneno haya kwa imla ya Yeremia - hii ilikuwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, na alisema, “Yahwe, Mungu wa Israel, asema hivi kwako, Baruku: Umesema, Ole mimi, kwa kuwa Yahwe ameongeza uchungu wa maumivu. Kuugua kwangu kumenichosha; sipati pumziko.' Hivi ndivyo unapaswa kusema kwake: “Yahwe asema hivi: Ona, nilichojenga, sasa ninararua chini. Nilichopanda, sasa ninangoa. Hii ni kweli juu ya dunia. Lakini unategema mambo makubwa kwa ajili yako? Usitegemee hayo. Uone, maafa yanakuja kwa binadamu wote - hii ni tamko la Yahwe - lakini ninakupa maisha yangu kama nyara popote utakakoenda.”

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.