Skip to content
BibleKenya

Biblia Takatifu

Isaya 20

Katika mwaka ambao Tartani alipofika kwa Ashdodi, alipotumwa na Sarjoni mfalme wa Asiria, nae akapigana na Ashdodd na akachukua. Mda huo Yahwe alizungumza na Isaya mwana wa Amozi, ''Nenda ukaondoe nguo za magunia katika kiuno chako, na ondoeni viatu vyenu kwenye miguu.'' Alifanya hivyo, tembeeni uchi na miguu wazi. Yahwe asema, ''Kama ilivyokuwa kwa mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na pasipo kuvaa viatu kwa miaka mitatu, ni ishara na dalili kuhusu Misri na kuhusu Ethiopia— katika njia hii mfalme wa Asiria atawaongoza mateka wa Misri, na walioko uhamishoni Ethiopia, watoto kwa wazee, waliouchi na wasio na viatu, na ambao hawajajisitiri kuiweka Misri katika aibu. Watafadhaika na kuona aibu, kwa sababu ya Ethiopia ni matumaini yao na Misri ni utukufu wao. Wenyeji wa pwani hiiwatasema siku hiyo, 'Kweli, hichi ndicho chanzo chetu cha matumaini, tulipokimbilia kuhitaji msaada kutoka kwa mfalme wa Asiria, je ni kwa jisi gani tunaweza kupona?''

Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.

Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.

BibleKenya

Reader settings

Theme
Font
Alignment
Reading width

Saved in this browser and used offline too. Press ? for keyboard shortcuts.