Biblia Takatifu
Zaburi 15
Tap a verse to save, highlight, add a note or share it.
Zaburi ya Daudi. Yahwe, ni nani atabaki hemani mwako? Ni nani atakaye ishi kwenye mlima wako mtakatifu? Yeyote anaye tembea bila lawama, yeye hufanya kilicho haki na huongea ukweli kutoka moyoni mwake. Yeye huwa hakashfu kwa ulimi wake, hawadhuru wengine, na hamtusi jirani yake. Mtu asiye na maana hudharauliwa machoni pake, bali yeye huwaheshimu wale wanao mhofu Yahwe. Yeye huapa kwa hasara yake mwenyewe na habadilishi ahadi yake. Yeye habadilishi nia yake aazimapo fedha. Yeye hachukui rushwa ili kumshuhudia kinyume asiye na hatia. Yeye afanyanyaye mbambo haya hatatikisika kamwe.
Swahili Unlocked Literal Bible / Biblia Takatifu. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Translation and contributors: see the complete source notice below. Licensed under CC BY-SA 4.0. Typeset from the source USFM; no intended changes to scripture wording.
Full source notice & licence · CC BY-SA 4.0 · SourceEdition imported 2026-10-25.